Jumapili 8 Machi 2026 - 16:48
Kulihami Taifa dhidi ya Marekani na Israeli ni wajibu wa kisheria na kiakili/ Kudhoofisha vikosi vya Jeshi ni haramu kisheria

Hawza/ Naibu Raisi wa Jumuiya ya walimu wa Hawza ya Qum, amefafanua kuwa: Kulilinda Taifa dhidi ya uvamizi wa adui Marekani na Utawala wa Kizayuni, ni wajibu kiakili, kisheria na kikanuni, na kulihami huku Taifa hakuhitajii idhini ya mtu yeyote yule na hakuna mtu mwenye haki ya kuzuia.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Abass Ka'bi katika ujumbe wake alisema kwamba; kulihami Taifa dhidi ya uvamizi wa adui Marekani na Utawala wa Kizayuni ni wajibu kiakili, kisheria na kikanuni na akasisitiza kuwa: Kwa msingi huu, kuvipa nguvu vikosi vya jeshi ni wajibu kisheria na kuvidhoofisha hivyo huhesabiwa kuwa ni haramu.

Katika ujumbe huo imekuja hivi:


بسم الله الرحمن الرحيم

Kulihami Taifa dhidi ya uvamizi wa adui Marekani na Utawala wa Kizayuni ni wajibu kiakili, kisheria na kikanuni na kufanya jambo lolote lile kwa namna yeyote ile iwezekanayo na kwa uwezo wote ni lazima, kulihami Taifa hakuhitajii idhini ya yeyote yule na mtu hana haki ya kumzuia mwenzake.

Kwa msingi huu, kuvipa nguvu vikosi vya jeshi ni wajibu kisheria na kuvidhoofisha hivyo huhesabiwa kuwa ni haramu.

Nguvu yeyote ile ya uvamizi iwe ni Marekani au Wazayuni, kwa hali yeyote ile na muda na mahala popote pale, ni lazima kukabiliana nayo ili kulilinda Taifa.

Wanadiplomasia katika kipindi cha uvamizi inabidi diplomasia zao ziwe ni za muqawama na jiahadi, na wawe ni wenye kuvipa nguvu vikosi vya jeshi.

والله المستعان
حسبنا الله ونعم الوكيل
نعم المولى ونعم النصير
عباس كعبي
١٦/١٢/١٤٠٤ - 7/3/2026

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha